Ubaguzi wa Makazi Kulingana na Rangi Unaonekanaje?

Makala hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2022


Mnamo tarehe 18 Juni, 2021, Marekani ilitambua Juneteenth kama likizo ya shirikisho kwa mara ya kwanza. Hapa New Hampshire mwaka 2022, sherehe zilifanyika kote jimboni ili kutambua siku hiyo na kusherehekea michango ya watu Weusi kwa jimbo katika historia yake yote.

Siku hii pia ni fursa ya kutafakari kuhusu kikwazo ambacho watu Weusi nchini Marekani wanakumbana nacho katika kupata ufikiaji sawa wa haki kadhaa, ikiwemo kupiga kura, mishahara sawa na makazi ya haki. Mradi wa Makazi ya Haki wa NHLA unafanya kazi ili kuhakikisha watu wote wanapata nyumba kwa usawa, ikiwemo matabaka hayo yaliyolindwa chini ya sheria. Matabaka haya ni pamoja na mbari, rangi, asili ya kitaifa, dini, jinsia, hali ya kifamilia, ulemavu, umri, mwelekeo wa kingono, hali ya ndoa na utambulisho wa kijinsia.

Ubaguzi wa makazi kulingana na mbari unaweza kuwa wazi, lakini pia unaweza kosa kuwa wazi sana. Unaweza kutokea kisiri na kuwa sababu katika maamuzi yaliyofanywa na wamiliki wa nyumba au wakopeshaji ambayo waathiriwa huenda wasitambue kuwa yametokea. Hapa, tutajadili njia tofauti ambazo watoa huduma za nyumba wamebagua kulingana na rangi na jinsi aina hii ya ubaguzi inaweza kuonekana.

Historia ndefu kuhusu Ubaguzi wa Rangi

Kukataza watu Weusi kupangisha au kununua nyumba katika maeneo fulani kumekuwa na athari za muda mrefu kwa uwezo wa Waamerika Waafrika kupata shule nzuri na kujenga utajiri wa kizazi. Leo, watunga sera wanajitahidi kuondoa tofauti hizi zilizo kwenye kumbukumbu; hata hivyo, ubaguzi wa rangi bado unaendelea, kama vile athari za kudumu kutoka kwa vizazi vilivyopita.

Utafiti wa mwaka 2020 uliofanywa na Habitat for Humanity kuhusu tofauti za kimbari katika makazi ulibainisha kwamba:

“Sera hizi za makazi za kibaguzi zimeunganishwa ili kukandamiza sana kaya za Watu Weusi, na kuwa na athari za kudumu, kati ya vizazi. Kutojumuishwa kwa misingi ya rangi kutoka kwa mipango ya shirikisho ya rehani, mikopo ya benki na jumuiya zilizo na fursa za kielimu na usawa za kujenga kulimaanisha kwamba wazazi Weusi walikuwa na utajiri mdogo wa kuwapa watoto wao ili kusaidia na malipo ya kwanza.

Watoto weusi walilelewa kukiwa na fursa nyingi zisizo sawa za kielimu katika shule na vitongoji visivyo na usawa. Wazazi weusi hawakuweza kufadhili masomo ya chuo kikuu ya watoto wao kwa usawa wa nyumbani, na hivyo kuchangia deni kubwa la wanafunzi Weusi waliohitimu kutoka vyuo, ikiwa si viwango vya chini vya kukamilisha masomo. Athari hizi za vizazi zinachangia sana katika kuelezea tofauti za kimbari tunazoziona leo katika utajiri, mapato na matokeo ya kielimu kwa Waamerika Waafrika.”

Ilitoa suluhisho kadhaa za sera, ikiwemo kuongeza usaidizi wa malipo ya kwanza kwa wanunuzi Weusi wa nyumba na kuongeza ufikiaji wa mikopo ya bei nafuu kwa wanunuzi Weusi wa nyumba na kushughulikia ugawaji wa eneo unaochochewa na ubaguzi wa rangi.

Mifano ya Ubaguzi wa Rangi

Ubaguzi wa rangi katika makazi huenda usiwe mwingiliano wa ana kwa ana. Hapa kuna mifano ya ubaguzi usio dhahiri.

● Mtu Mweusi anazungumza na mwenye nyumba kuhusu nyumba inayouzwa na anaalikwa kuzuru jengo hilo. Mara tu anapofika, mwenye nyumba anamjulisha mpangaji mtarajiwa kuwa nyumba hiyo imechukuliwa, wakati kwa kweli bado inapatikana.

● Mwombaji mwombaji Mweusi anayefuzu anakatazwa kupata nyumba kwa sababu ameorodhesha jina la kitamaduni la Waamerika Waafrika kwenye ombi.

● Wakala wa nyumba awaondosha wanandoa Weusi kutotazama nyumba zinazolingana na vigezo vyao lakini ziko katika vitongoji vya watu weupe pekee.

● Mpangaji Mweusi anapata taarifa kwamba analipa kodi ya nyumba ya juu zaidi kuliko majirani zake wazungu kwenye nyumba kama hiyo.

● Msimamizi wa urekebishaji hutanguliza maombi ya ukarabati yanayotolewa na wapangaji wazungu kuliko yale ya wapangaji Weusi.

Tofauti Kati ya Mbari na Rangi

Maneno "mbari" na "rangi" yanatumiwa kubainisha matabaka yaliyolindwa chini ya sheria za Makazi ya Haki, lakini kuna tofauti gani? Pale ambapo mbari inarejelea jamii ya mtu mwenyewe iliyotambuliwa au jamii anayotambulika, rangi inarejelea ubaguzi kulingana na weupe au weusi wa ngozi yake.

Kunaweza kuwa na baadhi ya matukio ambapo mtu anayetafuta makazi si dhahiri ikiwa ubaguzi unatokana na rangi, lakini ni wazi kwamba ubaguzi kwa mtu huyo ni kwa kuwa ana ngozi nyeusi. Kunaweza pia kuwa na matukio ambapo mwenye nyumba hupangisha tu kwa Waamerika Waafrika wenye ngozi nyeupe, lakini si wale walio na ngozi nyeusi. Wakati fulani, ubaguzi unatokana na mbari na rangi.

Je, Unahitaji Msaada wa Kuwasilisha Malalamiko?

Iwapo unashuku kuwa umebaguliwa kwa sababu ya mbari, rangi au sababu nyingine inayolindwa na sheria, Mradi wa Makazi ya Haki wa NHLA unaweza kujibu maswali yako na kukusaidia kuwasilisha dai. Kumbuka, watu wanaweza kubaguliwa kulingana na mbari na rangi bila kujali mbari au rangi ya mwenye nyumba. Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye fairhousing-nh.org au piga simu 1-800-921-1115.