Nini cha Kufanya Wakati Lugha Ni Kizuizi cha Kupangisha Fleti
Ustadi mdogo wa Kiingereza haupaswi kumzuia mtu kupangisha fleti. Watu ambao hawazungumzi Kiingereza kama lugha yao ya msingi wanaweza kuwa na uwezo mdogo wa kuzungumza, kusoma, kuandika au kuelewa Kiingereza. Hii inajulikana kama ustadi mdogo wa Kiingereza (LEP).
Chini ya sheria za haki za makazi, ni kinyume cha sheria kubagua mtu kulingana na mbari, rangi au asili ya kitaifa. Maamuzi ya makazi ambayo yanatokana na ustadi mdogo wa Kiingereza kwa ujumla yanahusiana na mbari au asili ya kitaifa.
Mradi wa Makazi ya Haki wa NHLA uko hapa ili kujibu maswali kuhusu ubaguzi wa makazi kwa kila mtu, ikiwemo watu wenye ustadi mdogo wa Kiingereza. Tunatoa huduma kwa waathiriwa wa ubaguzi wa makazi na tutatoa wakalimani kwa watu wa LEP.
Huu ni Ubaguzi wa Makazi?
Sheria ya Haki ya Makazi (FHA) inakataza ubaguzi kwa misingi ya asili ya kitaifa katika nyumba za kibinafsi na zinazosaidiwa na shirikisho. Watoa huduma wote wa nyumba wanaopokea usaidizi wa kifedha wa shirikisho pia lazima watii Kichwa cha VI cha Sheria ya Haki za Kiraia. Ni lazima wachukue hatua zinazofaa ili kuhakikisha kwamba watu ambao wana ustadi mdogo wa Kiingereza wana ufikiaji wa maana kwa programu na shughuli, ambayo inamaanisha kutoa wakalimani kwa watu wa LEP na inaweza kujumuisha kutoa tafsiri ya hati muhimu, kama vile mikataba ya kupangisha, katika hali fulani.
Chini ya FHA, mwenye nyumba hawezi kutumia sharti linalohusiana na lugha kwa watu wa mbari au mataifa fulani au matangazo ya jumla kama vile "wapangaji wote lazima wazungumze Kiingereza." Lafudhi ya mtu na asili yake ya kitaifa vinahusishwa moja kwa moja. Ikiwa mwenye nyumba anakataa kupangisha kwa mtu anayezungumza Kiingereza kwa ufasaha lakini kwa lafudhi, huo pia ni ubaguzi haramu.
Ili kusaidia kuhakikisha ufikiaji wa maana wa programu na shughuli, Mpango wa Ustadi Mdogo wa Kiingereza wa shirikisho hutoa ufadhili wa kuunda na kukuza nyenzo zilizotafsiriwa na mipango mingine inayosaidia watu wenye ustadi mdogo wa Kiingereza kutumia huduma zinazotolewa na Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji (HUD).
Jinsi ya Kufanya Upangishaji wa Fleti Uwe Shwari
Kuna uwezekano kwamba, ikiwa hujui Kiingereza vizuri, una wasiwasi kuhusu kuwasiliana na mwenye nyumba. Hii inaeleweka, lakini kuna nyenzo ambazo zinaweza kurahisisha mchakato huo.
Ulizia mkalimani
Watoa huduma za nyumba zinazofadhiliwa na shirikisho lazima watoe usaidizi wa lugha kwa waombaji na wapangaji. Hakikisha umeomba mkalimani ikihitajika ili kuwasiliana na mwenye nyumba.
Weka kwa maandishi
Hakikisha kwamba umehifadhi mawasiliano yote yaliyoandikwa kutoka kwa mwenye nyumba wako kuanzia mwingiliano wa kwanza. Unapaswa pia kuomba habari kwa maandishi kutoka kwa mwenye nyumba yako. Kuwa na taarifa muhimu ambayo umepewa kwa maandishi hukuwezesha kupata wakati wa kutafuta njia ya kutafsiri na kujadiliana na mtu unayemwamini. Pia inaweka rekodi ya vitendo vyovyote vya mwenye nyumba ambavyo vinaweza kuwa haramu.
Kagua mkataba wako wa kupangisha kwa uangalifu
Mkataba wa kupangisha ni hati ya kisheria. Hakikisha kwamba umeelewa kikamilifu sera zilizo ndani ya mkataba huo wa kupangisha kabla ya kutia saini, ikiwemo muda wa notisi unaopaswa kutoa unapoondoka.
Jinsi NHLA inavyoweza kusaidia
Mradi wa Makazi ya Haki wa NHLA unakuza ufikiaji wa haki wa makazi na husaidia waathiriwa wa ubaguzi. Tunaweza kujibu maswali kuhusu sheria za haki za makazi za jimbo na shirikisho na tunaweza kukuwakilisha. Ikiwa ungependa kuzungumza nasi, piga simu kwenye 1-800-921-1115.